Zlatko ayakubali majembe Yanga, kuandaa kikosi cha maangamizi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Sep 2020
Zlatko ayakubali majembe Yanga, kuandaa kikosi cha maangamizi

Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic tayari ameanza majukumu yake kuelekea mikiki mikiki ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na michuano mingine

Krmpotic aliwashuhudia wachezaji wa Yanga kwa mara ya kwanza juzi kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir, mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 2-0

Mserbia huyo amekiri kuvutia na uwezo walioonyesha wachezaji wake, hata hivyo amesema anahitaji muda wa kutengeneza kikosi imara zaidi

"Nimeridhishwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. Hii ni mara ya kwanza kuwaona, tutahitaji muda wa kufanya kazi pamoja ili tuwe bora zaidi," alisema Zlatko

Juzi Yanga ilicheza na Aigle Noir huku baadhi ya wachezaji hasa wa kigeni wakiwa wamefanya mazoezi ya pamoja siku tatu tu

Lakini nyota hao walionesha maelewano na kuwapa matumaini mashabiki pengine huenda wasihitaji muda mrefu sana kuweza kupata muunganiko

Yanga inaanza mechi zake za ligi jijini Dar es salaam, mchezo wa kwanza wakicheza na Tanzania Prisons, Septemba 06

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’