Kubwa Kuliko kujenga uwanja Kigamboni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2020
Kubwa Kuliko kujenga uwanja Kigamboni

Mwaka jana klabu ya Yanga iliendesha tukio kubwa la hamasa lililofahamika kama KUBWA KULIKO lililokuwa maalum kwa ajili mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuichangia timu yao

Ajenda kubwa ya tukio hilo lilikuwa kukusanya fedha kwa ajili ya usajili wa msimu uliopita

Msimu huu Yanga inatarajiwa kuandaa tukio hilo kwa mara nyingine lakini safari hii kukiwa na ajenda tofauti

Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema ajenda ya tukio la Mwaka huu ni kukusanya fedha kwa ajili ya Ujenzi wa uwanja Kigamboni

Nugaz amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga wakae tayari kuchangia zoezi hilo ili kuhakikisha timu inakuwa na uwanja wake kabla ya msimu huu kumalizika

"Tutaandaa KUBWA KULIKO ya kihistoria zaidi ya ile tuliyofanya mwaka jana. Safari hii tutafanya kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wetu kule Kigamboni. Wanayanga wakae tayari kuichangia timu ili tutimize malengo yetu ya kumiliki uwanja mkubwa wa kisasa kule Kigamboni," alisema Nugaz

Wataalam tayari wamebuni mchoro wa uwanja wa Yanga Kigamboni ambapo mabingwa hao wa kihistoria watakuwa na viwanja viwili, Hostel na Academy ya Watoto, Gym pamoja na mahitaji mengine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’