Tunaanza upyaa, Jumapili hii Uwanja wa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2020
Tunaanza upyaa, Jumapili hii Uwanja wa Mkapa

Msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom (2020-21) unaanza mwishoni mwa wiki hii siku ya Jumapili kwa timu 18 kushuka viwanjani

Msimu huu idadi ya timu zimepungua kutoka 20 za msimu uliopita na sasa ni 18

Kila timu itacheza michezo 17 kila mzunguuko na kufanya idadi ya michezo yote kuwa 34

Huu ni msimu muhimu sana kwa mabingwa wa kihistoria Tanzania, klabu ya Yanga inayowania kuurejesha ubingwa Jangwani baada ya kuukosa kwa misimu mitatu

Kipaumbele msimu huu ni kutwaa ubingwa, hilo halina mjadala kutokana na usajili mkubwa uliofanywa na GSM

Kikosi kilichoundwa na GSM kina hadhi ya kimataifa kuanzia wachezaji mpaka kocha, hivyo msimu huu Yanga sio timu ya kuwania nafasi ya pili au ya tatu

Hesabu za ubingwa zitaanzia jijini Dar es salaam, mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons siku ya Jumapili, Septemba 06 na utapigwa saa moja jioni uwanja wa Mkapa

Huu ni mchezo ambao Yanga inahitaji matokeo ya ushindi ili kuanza msimu vizuri, mwanzo mbaya unaweza kuvuruga utulivu unaonekana baada ya kikosi kuundwa upya

Pamoja na ukweli kuwa kocha Zlatko Krmpotic atahitaji muda kuunda kikosi chake cha ushindi, kwa kushirikiana na kocha Msaidizi Juma Mwambusi, atapaswa kuchanga karata zake vyema ili kuhakikisha mechi hii ya kwanza alama zote tatu zinapatikana

Aidha kupungua kwa timu kutampa muda wa kuimarisha kikosi chake wakati ligi ikiendelea kwani ni wazi siku za mapumziko kutoka mechi moja kwenda nyingine zitaongezeka

Baada ya mchezo huo, mechi itakayofuata ni dhidi ya Mbeya City nayo itapigwa uwanja wa Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’