Yanga vs Tanzania Prisons, tukutane kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2020
Yanga vs Tanzania Prisons, tukutane kwa Mkapa

Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga kesho Jumapili wanajambo lao pale uwanja wa Mkapa wakikabiliwa na mchezo wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2020/21 dhidi ya Tanzania Prisons

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mazingira yake

Kwa Yanga ni mchezo ambao wanahitaji ushindi ili kuanza vyema kampeni ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Hata hivyo mara nyingi, Tanzania Prisons ni timu iliyojipambanua kutoa ushindani kwa vigogo wa soka nchini

Msimu uliopita Yanga ilifanikiwa kuchukua alama nne kati sita katika mechi baina yake na Prisons

Prisons wamebadili kocha ambapo sasa wananolewa na kocha Salum Mayanga ambaye alikuwa kocha wa Ruvu Shooting msimu uliopita

Ni huyu Mayanga ambaye msimu uliopita aliifunga Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa ligi akiwa na Ruvu Shooting

Hata hivyo msimu huu atakutana na Yanga tofauti kabisa, ni timu iliyosukwa upya

Pengine katika kikosi atakachokutana nacho kesho, hakitakuwa na mchezaji hata mmoja ambaye alicheza mechi ya msimu uliopita

Ni Yanga yenye malengo makubwa, Yanga ambayo imedhamiria kwelikweli kushinda ubingwa baada ya kuupoteza kwa watani zao kwa misimu mitatu mfululizo

Lakini pia, mchezo huo utakuwa kibarua cha kwanza cha kocha Zlatko Krmpotic ambaye alianza kuinoa Yanga tangu Jumatatu iliyopita

Krmpotic anafahamu kilichomleta Tanzania ni kutwaa ubingwa na sio vinginevyo. Wakati akiendelea kuimarisha timu yake, hatahitaji kuanza kuangusha alama mapema hivi

Wenyewe Wanayanga wanasema msimu huu wanataka burudani na magoli. Walifurahia burudani kwenye mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir wiki iliyopita na sasa wanataka Burudani kwenye ligi

Kesho pale kwa Mkapa, Wananchi wanatarajiwa kufurika kushuhudia burudani waliyoandaliwa na vijana wao katika mchezo wa kwanza msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’