Mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kujivunia usajiliwa winga Tuisila Kisinda aliyetua kwa mabingwa hao wa kihistoria akitokea klabu ya AS Vita ya DR Congo
Katika takribani dakika 90 alizoitumikia Yanga mpaka sasa, Tuisila ameonyesha ni mchezaji atakayekuwa chachu ya mafanikio ambayo Yanga wanaweza kuyapata msimu huu
Mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alicheza kwa dakika 45 tu, lakini kama angekuwa makini angeweza kufunga mabao mawili
Ni mchezaji mwenye kasi, huyu atawapa sana shida mabeki wa timu pinzani
Mwanzo wake ndani ya Yanga ni mzuri, Wanayanga watarajie mambo makubwa kutoka kwake
Tayari ameonyesha uwezo wake binafsi, kadiri atakavyokuwa akizoeana na wenzake, bila shaka mchango wake utaonekana zaidi katika timu
ADVERTISE HERE