Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu, kikosi cha Yanga, mwishoni mwa wiki siku ya Jumapili, kitashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo wa raundi ya pili
Huu ni mchezo ambao Yanga itahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kuhakikisha mahesabu ya kuwania ubingwa msimu huu yanaendelea kuwa salama
Yanga iliwapa matumaini mashabiki wake kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons kwa kutandaza kandanda safi licha ya kulazimishwa matokeo ya sare
Wengi wana imani mechi ya Jumapili mabingwa hao wa kihistoria hawana sababu ya kukosa alama tatu
Watakutana na Mbeya City ambayo mchezo wake wa kwanza ilibamizwa mabao 4-0 na KMC
Vijana wa kocha Zlatko Krmpotic wako 'chimbo' huko Kigamboni wakijiwinda na mchezo huo
Uongozi wa klabu ya Yanga umewataka Mashabiki wajitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo kuishangilia timu yao, lengo likiwa moja tu, kupata ushindi
Mechi za raundi ya pili zitaanza kupigwa kesho Ijumaa kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi
