Kuanzia saa nne na nusu leo Ijumaa, tukio kubwa la kihistoria litafanyika pale Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Kwanza kutakuwa na uzinduzi wa jezi mpya za mabingwa hao wa kihistoria kwa ajili ya msimu wa 2020/21
Lakini pia uzinduzi huo utakwenda sambamba na utambulisho wa duka rasmi la Yanga ndani ya Jengo la Makao Makuu ya klabu
Yanga inakuwa klabu ya kwanza kumiliki duka la aina hiyo katika jengo lake. Kuanzia leo Wananchi wataweza kujipatia bidhaa halisi za klabu yao katika duka hilo
Hii ni hatua muhimu kuelekea Taasisi imara ya Yanga itakayokuwa na uchumi imara
ADVERTISE HERE