Mashabiki wa Yanga walikuwa na shauku ya kumshuhudia kiungo kutoka Angola Carlos Fernandez 'Carlinhos' akiwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Hakika dakika zake 30 alizopewa na kocha Zlatko Krmpotic jana, alizitendea haki
Mpira yake mingi ilikuwa na madhara kwenye lango la Mbeya City
Muhimu zaidi, mguu wake ulizalisha bao pekee la Yanga akichonga kona maridhawa kwenye dakika ya 87 ambayo ilitua kichwani kwa Lamine Moro
Ni kiungo asiyekuwa na mambo mengi uwanjani, akili yake muda wote ni kupeleka mashambulizi mbele
Lakini pia, Carlinhos ameonesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu. Yeye na Mukoko wamejipambanua kuwa wataalamu wa mipira hiyo
Bado Krmpotic anasema Carlinhos hayuko fit kwani amekaa muda mrefu bila ya kucheza mpira kabla hajasajiliwa na Yanga kutoka Interclube ya Angola
Ligi ya Angola ilisimama kwa miezi sita na baadae kufutwa kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona
Huu ni mwanzo tu, bila shaka mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka kwake