Viungo Thabani Kamusoko na Papi Kabamba Tshishimbi hawamo kwenye kikosi kinachoivaa Tanzania Prisons mda mchache ujao kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Wachezaji hao bado ni majeruhi kulingana na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten.
Aidha mshambuliaji Amissi Tambwe naye hajajumuishwa kwenye kikosi hicho.
Tambwe amefanya mazoezi kamili na kikosi cha Yanga kwa takribani siku mbili tu.
Kabla ya hapo alikuwa akifanya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa Daktari kuhakikisha anarejea dimbani bila madhara.
Kocha George Lwandamina huenda ameamua asifanye bahati nasibu kwa kumpanga Tambwe kwenye mchezo wa leo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Kwa kawaida mchezaji aliyekaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi inashauriwa arejee dimbani taratibu.
Kutomtumia leo kunampa nafasi Tambwe kujiimarisha na kurejea katika hali yake kwa utimilifu zaidi.
Kwani ligi inatarajiwa kusimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Challenge inayoanza Disemba 03, 2017.

ADVERTISE HERE