Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema utaratibu wa kutoa bonasi kwa wachezaji wataendelea nao msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita lakini kuna maboresho
Msimu uliopita GSM walikuwa wakitoa bonasi ya fedha kwa kila mchezo wa ligi ambao Yanga walikuwa wakishinda
Hersi amesema msimu huu mabadiliko waliyofanya ni kutoa bonasi kwa kulingana na malengo yanayokuwa yamewekwa
"Msimu uliopita tulikuwa na bonasi katika kila mechi ilikuwa ukishinda basi unapata bonasi ila tukishindwa tulikuwa hatutoi pamoja na sare hakukuwa na bonasi"
"Msimu huu tunataka kugawa kutokana na pointi ambazo tutakuwa tunazitaka. Mfano kama malengo ni kuvuna alama 15 kutoka michezo mitano, tukifanikiwa kuzipata basi bonasi inakuwa kubwa.
"Lengo ni kuona kwamba katika pointi 15 ikitokea tukapata pointi 10 hapo bonasi itapungua na tukipata pointi tano nje ya pointi 15 hapo hatutatoa kitu," alisema
Utaratibu huo umeanza tangu mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons