Ukweli ni kwamba sasa nyota wa Yanga wanafurahia maisha katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria
Baada ya misimu mitatu ya machozi, jasho na damu, hatimaye msimu huu mwanga unaonekana dhahiri kuwa mambo mazuri yanakuja
Wachezaji 'wana-enjoy' maisha wakiwa kambini na hata wakiwa uwanjani wakitimiza majukumu yao
Shukrani za kipee wanastahili wadhamini, GSM, uongozi wa Yanga kwa kufanikiwa kuirejesha amani na furaha pale Jangwani
Kwani kwa nyuso hizi, ni wazi vijana wako tayari kukamilisha malengo ya msimu huu ambayo ni kutwaa ubingwa wa VPL





ADVERTISE HERE