FT : Yanga 2-0 Mlandege

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Sep 2020
FT : Yanga 2-0 Mlandege

Kikosi cha Yanga kimeondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mlendege Fc katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Ulikuwa ni mchezo ambao Yanga ingeweza kuondoka na ushindi mnono zaidi kama safu ya ushambuliaji ingeongeza umakini

Kwenye kipindi cha kwanza, kocha Zlatko Krmpotic alitumia kikosi tofauti akiwapa nafasi Waziri Junior, Said Juma Makapu, Abdulaziz Makame, Adeyum Saleh na wengine ambao hawaonekani mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Junior kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Mlandege kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari

Kipindi cha pili Krmpotic alibadili kikosi kizima, akiwaingiza nyota wote wa kikosi cha kwanza

Yanga iliendelea kutawala mchezo katika kipindi hicho wakifunga bao la pili kupitia kwa Tonombe Mukoko aliyepiga shuti kali nje ya 18

Mukoko na Zawadi Mauya walin'gara kwenye safu ya kiungo katika kipindi cha pili pengine Krmpotic huenda akawatumia pamoja mchezo dhidi ya Kagera Sugar siku ya Jumamosi

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi kuelekea mkoani Kagera tayari kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’