Krmpotic ataka mabao zaidi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2020
Krmpotic ataka mabao zaidi Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Kmpotic amesema bado timu yake haijafikia pale inapostahili licha kuonekana kuimarika

Jana Yanga licheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Waziri Junior na Mukoko Tonombe

Katika mchezo huo Yanga ilicheza kandanda safi lakini bado changamoto ilionekana kwenye eneo la ushambuliaji kosakosa zlikuwa nyingi

Krmpotic amesema bado haridhishwi na idadi ya mabao ambayo timu yake inafunga ukilinganisha na nafasi wanazotengeneza

"Tumecheza vizuri lakini bado ipo changamoto kwenye eneo la umaliziaji. Nafasi tunatengeneza lakini matumizi yamekuwa hafifu. Kama kocha siridhishwi na hali hii, tunapaswa kurekebisha makosa haya," alisema Krmpotic ambaye leo kikosi chake kimetua Bukoba tayari kuwakabili Kagera Sugar siku ya Jumamosi

Hata hivyo Mserbia huyo amesema anaamini safu yake ya ushambuliaji itakuwa sawa kwani baadhi ya wachezaji walikaa nje muda mrefu bila ya kucheza mpira tangu ligi zilipofutwa kutokana na changamoto ya corona

Yacouba Songne, Carlinhos na Michael Sarpong wote ligi walizokuwa wakicheza zilisimama tangu mwezi March na baadae kufutwa, hivyo walipotua Yanga hawakuwa fiti

Yanga jioni ya leo inafanya mazoezi yake ya kwanza Bukoba kujiandaa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’