Ratiba ya Ligi Kuu msimu huu imempa ahueni kocha mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic katika kukiandaa kikosi chake
Kupungua kwa timu kutoka 20 mpaka 18, kumeongeza muda wa mapumziko kati ya mchezo mmoja na mwingine
Sasa vilabu vinacheza mechi moja tu kwa wiki jambo ambalo linatoa wigo mpana kwa timu kufanya maandalizi
Krmpotic alitua Yanga wiki moja kabla ya ligi kuanza hivyo bado anahitaji kujenga kikosi chake kilichosheheni nyota wengi wapya
Kesho Jumamosi Yanga itashuka uwanja wa Kaitaba kumenyana na Kagera Sugar kisha wataelekea mkoani Morogoro ambako baada ya wiki moja watacheza na Mtibwa Sugar
ADVERTISE HERE