Bado Wanayanga hawajaiona 'combination' ya kikosi inayowajumuisha pamoja mawinga Tuisila Kisinda na Farid Mussa
Kocha Zlatko Krmpotic amewatumia wachezaji hao katika vikosi tofauti lakini upo uwezekano kesho wanaweza kuanza pamoja dhidi ya Kagera Sugar
Mashabiki wa Yanga wameonyesha kuwa na matumaini makubwa kwa wachezaji hawa ambao usajili wao ulitikisa
Tayari Kisinda amewapa mashabiki kile wanachotaka akifanikiwa kufunga bao mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir
Lakini pia Kisinda amekuwa msumbufu kwa walinzi wa timu pinzani, winga huyo tereza amedhihirisha hakabiki kwa urahisi

Farid bado hajapata muda mrefu wa kuonyesha makali yake kwenye kikosi ikielezwa kuwa winga huyo bado hayuko fiti
Ikumbukwe Farid amerejea nchini akitokea Hispania alikokuwa akicheza timu ya Tennerife inayoshiriki lig daraja la pili
Alikuwa nje ya uwanja tangu Hispania iliposimamisha shughuli zote za michezo kutokana na janga la corona
Ameendelea kuimarika, hakuna shaka wanayanga wasubiri mambo mazuri kutoka kwake