Kikosi cha Yanga kiko mkoani Kagera ambapo saa kumi jioni watashuka kwenye uwanja wa Kaitaba kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Katika kipindi cha miaka mitano, Yanga imeandikisha mwenendo mzuri wa matokeo ikishinda michezo yote iliyochezwa katika uwanja huo
Ushindi wa mwisho ni msimu uliopita, mabingwa hao wa kihistoria wakiondoka na ushinda wa bao 1-0
Tangu mwaka 2016, Kagera Sugar haijawahi kupata hata alama moja dhidi ya Yanga katika michezo iliyochezwa katika uwanja wake
Leo miamba hao wanakutana katika mchezo mwingine wa kukata na shoka
Kikosi cha Yanga kiliwasili Kagera juzi, jana wakakamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa kumi Alasiri
Pamoja na mabadiliko makubwa ya kikosi, Yanga inaonekana kuwa imara zaidi kuliko wapinzani wao na pengine leo wanaweza kuendeleza uwamba wao katika uwanja wa Kaitaba