Muhimu kwetu ni ushindi - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Sep 2020
Muhimu kwetu ni ushindi - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema walihitaji alama tatu katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar jambo ambalo wamelifanikisha

Akizungumza baada ya mchezo uliopigwa mkoani Kagera jana, Hersi amesema timu yoyote inaposhuka uwanjani kusudio la kwanza ni kushinda mengine huja baadae

"Sisi tulihitaji pointi tatu, tumezipata hayo mengine yatakuja baadae. Misimu miwili nyuma Real Madrid walitwaa ubingwa wa Ulaya dhidi ya Liverpoopl lakini hawakucheza mpira mzuri. Ilikuwa hivyo hivyo kwa Liverpool dhidi ya Tottenham, jambo muhimu hapa ni pointi tatu"

"Timu yetu bado ni mpya, kocha anaendelea kuwaunganisha wachezaji, wakati utafika kila kitu kitakuwa sawa," alisema Hersi

Baada ya ushindi huko Kagera, Yanga inarejea jijini Dar es salaam leo kuanza maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Septemba 26 mkoani Morogoro

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama saba, msimamo unaweza kubadilika kutegemea na matokeo ya mechi zitakazopigwa leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’