Kocha Mkuu wa Yanga Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ametoa wiki moja ya mapumziko kwa wachezaji wake kufuatia mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu ikiwa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam.
Taarifa iliyotolewa na Yanga SC jioni ya leo imesema kwamba kocha Lwandamina ametoa siku saba za mapumziko kwa wachezaji wake kuanzia leo Jumatatu kikosi kitarejea tena mazoezini Jumatatu ijayo.
Yanga inakwenda mapumzikoni ikitoka kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu juzi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mapumziko hayo hayawahusu wale waliotwa kwenye timu za Taifa kwa ajili ya michuano ya Chalenji.
Hao wanakwenda kujiunga na timu zao za Taifa tayari kwa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Disemba 03.

ADVERTISE HERE