Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Jamhuri
Yanga iliwasili mkoani Morogoro mapema jana na jioni wakaanza mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri
Hafidh amesema wanatarajia upinzani mkali kutoka kwa Mtibwa Sigar kwani ni kawaida kwa timu hiyo inapocheza na Yanga hasa mkoani Morogoro mchezo huwa ni mgumu
Hafidh amesema makocha walipata nafasi ya kuisoma Mtibwa Sugar kupitia michezo yao waliyocheza msimu huu hivyo wako tayari kukabiliana nao
"Huu ni mchezo muhimu kwetu, tumekuja mkoani Morogoro kusaka ushindi. Tunafahamu hautakuwa mchezo rahisi kwani hata wapinzani wetu wamejipanga na mara nyingi tukikutana nao hapa mchezo huwa hautabiriki"
"Walimu walipata nafasi ya kuangalia mechi zao zilizopita na kujua uwezo wa kila mchezaji, hatutazubaa, tutaongeza umakini wakati wote wa mchezo," alisema Hafidh
Yanga inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama saba baada ya kushuka dimbani mara tatu
Ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar utawahakikishia kupanda nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa ligi