FT : Yanga 2-0 KMKM

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2020
FT : Yanga 2-0 KMKM

Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Mcongomani Mukoko Tomombe ameendeleza makali yake katika kupachika mabao akifunga mabao yote mawili

Bao la kwanza alilifunga kwa kichwa kwenye dakika ya 11 akimalizia kwa kichwa kona ya Carlinhos

Makosa ya safu ya ulinzi yalimpa Mukoko nafasi ya kuongeza bao la pili kwa shuti la chinichini kwenye dakika ya 31

Yanga ilitengeneza nafasi nyingi kwenye kipindi cha kwanza, bado umaliziaji ni changamoto

Katika kipindi cha pili kocha Zlatko Krmpotic alibadili kikosi alichoanza nacho

Kuingia kwa viungo Haruna Niyonzima, Feisal Salum na Zawadi Mauya kuliiwezesha Yanga kutawala eneo la kiungo lakini changamoto ilibaki katika kutengeneza nafasi za mwisho

Yanga imetumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’