FIFA inamtambua Morrison kuwa mchezaji wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2020
FIFA inamtambua Morrison kuwa mchezaji wa Yanga

Kama ulidhani ukimya wa Yanga kuhusu sakata la winga Bernard Morrison ulimaanisha kushindwa basi ulijidanganya kwani uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria umelitaka shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwanyan'ganya Simba pointi za mechi zote walizomtumia Morrison kwani hana mkataba halali na klabu hiyo

Akizungumza na wanahabari jioni ya leo Alhamisi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wamebaini mapungufu kadhaa kwenye mkataba wa Morrison na Simba

Mwakalebela amesema katika mkataba huo uliosainiwa August 14, 2020 hakuna mahali ambapo klabu ya Simba imesaini kuuhalalisha

Lakini pia Mwakalebela amesema wamepata uthibitisho kuwa mkataba wa Morrison na Yanga bado unatambulika FIFA na hata sasa mfumo wa usajili wa FIFA 'TMS' unamtambua Morrison kuwa mchezaji wao halali

Uongozi wa Yanga umeiandikia barua TFF wakiitaka waichukulie hatua klabu ya Simba kwa kumtumia mchezaji ambaye hawana mkataba halali nae

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’