Kikosi cha Yanga kesho Jumamosi kitashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom raundi ya tano
Baada ya ushindi katika michezo mitatu iliyopita, Yanga imepania kuendeleza mwendo wa kuokota alama tatu kila inaposhuka dimbani
Mabingwa hao wa kihistoria wana hesabu kali msimu huu, wanataka ubingwa wa ligi kuu walioupoteza kwa msimu mitatu mfululizo
Mfisa Mhamasishaji, Msemaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kwenye mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku
Viingilio vya mchezo huo, Mzunguko 5,000, VIP B&C 10,000 na VIP A 15,000
ADVERTISE HERE