Dakika 180 ngumu kwa Krmpotic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Oct 2020
Dakika 180 ngumu kwa Krmpotic

Kesho Kocha Mkuu wa Yanga Zlatko Krmpotic atakuwa na nafasi ya kutuliza presha ya mashabiki pale kikosi chake kitakapochuka dimbani kuikabili Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Mserbia huyo ametimiza mwezi mmoja tangu aanze kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria

Hata hivyo pamoja na timu yake kufanya vizuri, bado mashabiki hawaonekani kuridhishwa na kiwango cha timu yao

Tayari kuna majina yanazungumzwa, hivyo ni wazi Krmpotic atahitaji kuhakikisha timu yake inapata ushindi hasa katika michezo miwili inayofuata

Baada ya mchezo wa Coastal Union, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba

Kama Yanga haitashinda dhidi ya Coastal Union halafu pia ikakosa ushindi dhidi ya Simba, ni wazi nafasi ya Krmpotic kubaki Yanga itakuwa finyu

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM haukutosha kuwapa furaha mashabiki wengi wanaotamani kuiona timu yao ikipata ushindi mnono zaidi

Juma Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi, alisema kuwa walitumia mchezo huo kuangalia namna ambavyo timu yao inapaswa kucheza

Mwambusi amewahakikishia mashabiki kuwa timu yao inaendelea kuimarika, wakati utafika watafunga idadi kubwa ya mabao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’