Matheo ruksa kuondoka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2017
Matheo ruksa kuondoka Yanga
Lipuli na Kagera Sugar zimekuwa zikipigana vikumbo kuwania sahihi ya mshambuliaji wa Yanga Matheo Antony ambaye kocha wake George Lwandamina ameridhia aondoke kwa mkopo.

Kagera Sugar iko katika nafasi nzuri zaidi ya kumnyakua Matheo ambaye kwa sasa yuko kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes kinachojiandaa na michuano ya Chalenji inayoanza nchini Kenya wiki ijayo, Disemba 03.

"Bado nipo kwenye mazungumzo na uongozi ili kujua haki za msingi ambazo atazipata mchezaji na klabu pia pindi tutakapomtoa kwa mkop,"amesema Lwandamina.

"Unajua huyu mchezaji ni mali ya klabu kwahiyo nilazima tuhakikishe kila upande unafaidika na zoezi ambalo linakwenda kufanyika."

Matheo mwenye umri wa miaka 22 alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumika Yanga mwezi Julai, 2017.

Hata hivyo ameshindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga akiambulia kucheza katika michezo ya kirafiki pekee.

Mbali na Matheo, Yusuph Mhilu na Maka Edward nao wanawaniwa kusajiliwa kwa mkopo na Mbao FC.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’