Wakati wowote Yanga itamuweka hadharani mrithi wa Zlatko Krmpotic ambaye mtihani wake wa kwanza utakuwa mchezo dhidi ya Simba Oktoba 18
Juzi baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union Yanga ilitangaza kumfuta kazi Krmpotic licha ya Mserbia huyo kushinda mechi nne kati ya tano alizocheza kwenye ligi
Uamuzi huo unatoa taswira kuwa kwa muda aliokaa na timu Krmpotic hakuonyesha kuwa na uwezo wa kuifikisha Yanga 'nchi ya ahadi'
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amesema watatumia kipindi cha mapumziko ya kalenda ya FIFA kujiandaa vyema kuelekea mchezo dhidi ya Simba huku akibainisha kuwa watamtangaza mrithi wa Krmpotic wakati wowote
Makocha watatu wamekuwa wakitajwa zaidi, Mjerumani Ernst Middendorp aliyekuwa kocha wa Kaizer Chiefs, George Lwandamina aliyekuwa kocha wa Zesco United na Cedric Kaze mtaalam wa soka kutoka Academy ya Fc Barcelona
Jana Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alidokeza kuwa Kaze ana nafasi kubwa ya kukabidhiwa mikoba ya Krmpotic
Kocha huyo mpya atakuwa na wiki mbili za kukiandaa kikosi chake kabla ya kuikabili Simba