Dk Msolla awapa ujumbe mzito wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Oct 2020
Dk Msolla awapa ujumbe mzito wachezaji Yanga

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wachezaji wa klabu hiyo kusimama imara kuhakikisha wanatimiza malengo yaliyowekwa msimu huu

Aidha Dk Msolla amewataka wachezaji wasitetereshwe na mabadiliko ya benchi la ufundi yaliyofanyika, kwani hilo ni jambo la kawaida

Uongozi wa Yanga ulizungumza na wachezaji baada ya kuchukua uamuzi wa kumfuta kazi kocha Zlatko Krmpotic ambaye alidumu katika nafasi yake kwa siku 37 tu

"Kuondoka kwa kocha hakupaswi kuwatia unyonge, muhimu tunaamini katika uwezo wenu hivyo muendeleze kazi nzuri wakati huu ambao anatafutwa kocha mkuu mwingine"

"Mnafahamu kuwa timu inayohitaji mafanikio na inayojijenga kuna wakati inapitia katika hatua ngumu kama hizi . Kusudio letu ni kuona kwa pamoja tunaweza kufikia malengo tuliyojiwekea msimu huu" alisema

Yanga kwa sasa iko chini ya kocha msaidizi Juma Mwambusi aliyepewa jukumu la kuiandaa timu wakati kocha mkuu akisubiriwa kuwasili

Cedric Kaze raia wa Burundi ndiye anayetajwa kurithi mikoba ya Krmpotic

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’