Kikosi cha Yanga jioni ya leo majira ya saa moja usiku kitashuka kwenye uwanja wa Azam Complex, kupimana ubavu na Mwadui Fc katika mchezo wa kirafiki
Wakati huu ambao ligi imesimama ni fursa kwa makocha kuviweka sawa vikosi vyao tayari kwa mikiki pale ligi itakaporejea wiki ijayo
Kwa Yanga kocha Msaidizi Juma Mwambusi atatumia mchezo huo kujaribu mbinu mpya akiwa amerithi kwa muda mikoba iliyoachwa na Mserbia Zlatko Krmpotic
Mfumo uliokuwa ukitumiwa na kocha huyo haukuwafurahisha wengi na ndio sababu kuu iliyomfanya aondoshwe baada ya siku 37 tu
Hivyo kuanzia mchezo wa leo, Wanayanga wanatarajia kuiona Yanga inayoshambulia zaidi pamoja na kufunga mabao mengi
Viingilio vya mchezo huo VIP ni Tsh 5,000/- wakati mzunguuko ni Tsh 3,000/-. Tiketi zitauzwa uwanjani
Aidha, katika mchezo huo Yanga itawakosa nyota wake watano ambao wanakabiliwa na majukumu ya timu za Taifa
Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto, Feisal Salum na Ditram Nchimbi wao wako katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakati Haruna Niyonzima yeye yuko na timu ya Taifa ya Rwanda