Kaze asubiriwa mwishoni mwa wiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2020
Kaze asubiriwa mwishoni mwa wiki

Wanayanga tayari wamesikia taarifa kuwa Cedric Kaze raia wa Burundi ndiye anayesubiriwa kuja kuchukua mikoba iliyoachwa na Mserbia Zlatko Krmpotic. Hata hivyo bado haijaelezwa na uongozi ni lini kocha huyo atawasili

Habari njema ni kuwa Kaze anaweza kutua wikiendi hii kuanza majukumu yake ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amedokeza walikuwa wakikamilisha mambo ya msingi na kocha huyo na wanatarajia anaweza kuwasili wakati wowote kuanzia wikiendi hii

Inaelezwa Kaze anafanya mawasiliano na kocha Msaidizi Juma Mwambusi, lakini pia amepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wachezaji wa Yanga

Jambo jema zaidi ni kuwa Kaze hatakuwa mgeni na kikosi hiki cha Yanga kwani alishiriki katika michakato ya baadhi ya usajili wa wachezaji hasa wa kigeni kabla ya kupata udhuru mwanzo uliomfanya ashindwe kutua nchini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
52m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’