Wengi wanajiuliza kwa nini uongozi wa Yanga umemrejea kocha Cedric Kaze baada ya kumtimua aliyekuwa kocha mkuu Zlatko Krmpotic
Imekuwa sio rahisi kwa Yanga kumpata Kaze lakini wamefanikiwa na sasa inaelezwa wiki hii haimaliziki Kaze atakuwa ametua nchini kuanza majukumu yake
Imebainika kuwa kocha huyo raia wa Burundi ndiye aliyehusika kwenye usajili wa nyota wote wa kigeni isipokuwa Carlinhos tu
Mwenyewe amethibitisha kuwa wachezaji Mukoko Tomombe, Tuisila Kisinda, Yacouba Sogne na Michael Sarpong ni wachezaji alioidhinisha wasajiliwe baada ya kujiridhisha na uwezo wao
Ikumbukwe Kaze alipaswa kuwa kocha wa Yanga kabla ya Krmpotic, alishindwa kutua nchini mwanzoni baada ya kupata matatizo ya kifamilia
"Ni kweli nimehusika kwenye usajili wa wachezaji Mukoko Tomombe, Tuisila Kisinda, Michael Sarpong na Yacouba Songne, hawa ni wachezaji ambao niliwafuatilia kwa muda mrefu"
"Mchezaji pekee ambaye sikuwa na taarifa zake sahihi ni Carlinhos, lakini baada ya kumuona kwenye mechi alizocheza msimu huu, nimejiridhisha ni mchezaji ambaye atakuwa na mchango mkubwa kwa timu yetu," alisema Kaze
Kaze anatarajiwa kutua Alhamisi ya wiki hii kuanza majukumu kunako mabingwa hao wa kihistoria