Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema kiungo mshambuliaji Said Ntibanzonkiza aliyesajiliwa na Yanga jana, ataanza kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria Novemba 15
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 alisaini mkataba wa miezi 18 ikiwa ni siku moja baada ya kuitungua Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi
Usajili wake unatajwa kuwa pendekezo la kocha wa Yanga Cedric Kaze anayetarajiwa kuwasili nchini siku chache zijazo
Ntibazonkiza ni mchezaji mzoefu, amecheza ligi kuu kule Uturuki, Poland, Uholanzi na Ufaransa
Alizaliwa May 1, 1987 pale Bujumbura-Burundi, karia yake ya soka ilianza pale Vital'O mwaka 2003 hadi 2004
Mwaka 2006 alijiunga na NEC Nijmegen ya nchini Uholanzi akianzia kwenye timu ya vijana na mwaka huo huo 18 Novemba akapandishwa timu ya wakubwa ambako alidumu mpaka mwaka 2010 na kufanikiwa kucheza mechi 70 na kupachika magoli 10
Mwaka 2010 alijiunga na klabu ya KS Cracovia ya nchini Poland ambako alidumu mpaka mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza michezo 85 na kutupia magoli 17
Mwaka 2014 alijunga na klabu ya Akhisar Belediyespor ya nchini Uturuki ambako alidumu mpaka mwaka 2015 na kucheza michezo 13 na kupachika goli 1
Mwaka 2015 alijiunga na Caen Fc ya nchini Ufaransa ambayo kwa wakati ule ilikuwa inashiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) huku alipelekwa timu B (Caen B) ambako alicheza mechi 4 na kufunga goli 1
Mwaka huo huo 2015 alipandishwa Senior team Caen Fc ambako alidumu mpaka mwaka 2016 na kufanikiwa kucheza mechi 14 na kufunga goli 1
Mwaka 2017 alijunga na klabu ya FC Kaisar ya nchini Khazakistan ambako alicheza msimu mmoja tu na kufanikiwa kucheza mechi 10 na kufunga magoli mawili
Baadae aliachana na klabu hiyo na kuwa mcheza huru ambapo mwaka 2019 timu yake ya zamani Vital'O iliamua kumrudisha ndani ya kikosi cha Warundi hao
Upande wa timu ya Taifa, Ntibazonkiza ni nahodha wa kikosi cha Burundi tangu mwaka 2010, akiitumikia timu hiyo mechi 13 akifanikiwa kufunga mabao matano
Yanga imesheheni wachezaji wengi vijana wenye kiu ya mafanikio, ujio wa Ntibazonkiza, mchezaji mwenye uzoefu tena wa soka la Kimataifa ni wazi utawaongezea kitu