Juzi Jumapili, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alipaswa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili TFF kilichofanyika jijini Dar es salaam
Hata hivyo Mwakalebela ameeleza kushangazwa na wito huo ambao haukutaja sababu ya kuitwa kwake
Alishindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa alikuwa nje ya mkoa wa Dar es salaam
"Nimepokea wito bila hati ya mashitaka jambo ambalo ni kinyume na kanuni za maadili. Lakini bahati mbaya nilikuwa nje ya Dar es Salaam kwa matatizo ya kifamilia , hivyo nimewaomba TFF wanipangie tarehe nyingine"
"Lakini pia nimeomba wanieleze shauri langu linahusu jambo gani ili nijipange katika utetezi au katika mazungumzo" amesema Mwakalebela
Mwakalebela aliitwa siku moja kabla ya kusikilizwa kwa shauri la Bernard Morrison ambalo uongozi wa Yanga ulilifungua wakipinga mkataba wa Mghana huyo na klabu ya Simba
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilitarajiwa kusikiliza shauri hilo siku ya jana Jumatatu, bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu yaliyojiri