Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina yuko nchini Zambia kwa mapumziko kufuatia kusimama kwa ligi kuu ya Vodacom kupisha michuano ya Chalenji inayoanza nchini Kenya Disemba 03.
Lwandamina alitoa mapumziko ya siku saba kwa wachezaji wake huku yeye akitumia siku hizo kwenda Zambia.
Mzambia huyo anatarajiwa kurejea wikiendi hii tayari kuongoza mazoezi ya kikosi chake yanayoanza Jumatatu, Disemba 04.
Aidha Yanga inatarajiwa kuwafanyia majaribio washambuliaji watatu wa Kimataifa ambapo mmoja kati yao huenda akasajiliwa kama ataweza kulishawishi benchi la ufundi
Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa Disemba 15 na tayari Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wawili Fiston Kayembe Kanku na Yohana Mkomola.
Kabla hajaondoka kwenda Zambia wiki iliyopita, Lwandamina alisema hakusudii kusajiliwa wachezaji wengi wakati huu wa dirisha dogo la usajili.
Alisema ataongeza wachezaji wachache katika kikosi chake hasa kwenye nafasi zenye upungufu.
Usajiliwa Fiston Kayembe kutoka DRC Congo umelenga kuimarisha safu ya ulinzi huku Mkomola, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka timu ya Taifa ya vijana akiongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.
Mkomola yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Heroes kinachoshiriki michuano ya Chalenji nchini Kenya.

ADVERTISE HERE