KMC vs Yanga, hii ni mechi ya kisasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2020
KMC vs Yanga, hii ni mechi ya kisasi

Keshokutwa Jumapili Yanga itakuwa jijini Mwanza ambapo saa kumi Alasiri watashuka uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

KMC wamepeleka mchezo huo kule Mwanza, wakiamini watakuwa na nafasi ya kupata ushindi dhidi ya Yanga inayoendelea kuimarika chini ya kocha Cedric Kaze

Kuelekea mchezo huo, wachezaji wa Yanga wana deni kubwa kwa mashabiki wao ambao bado wana kumbukumbu ya matokeo ya msimu uliopita

Yanga iliambulia alama moja tu dhidi ya KMC. Msimu uliopita mchezo wa kwanza ukimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 huku KMC wakishinda mchezo wa pili kwa bao 1-0

Hii ni mechi ya kisasi kwa Yanga tena inapigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambao kwa Yanga ni kama nyumbani tu

Yanga ina utajiri mkubwa wa mashabiki mkoani Mwanza, Wananchi watajitokeza kwa wingi kuwapa sapoti wachezaji wao

Lakini pia, huu ni msimu ambao hesabu za Yanga ziko kwenye ubingwa tu. Ushindi ndio matokeo ambayo Wananchi wanahitaji

KMC walianza msimu vizuri lakini wametetereka baada ya mechi tatu za mwanzo. Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’