Carlinhos apewa program maalum Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Oct 2020
Carlinhos apewa program maalum Yanga

Kwa takribani wiki moja, kiungo fundi Carlinhos amekosa mazoezi ya kikosi cha Yanga na kumfanya asiwe sehemu ya kikosi kilichoikabili Polisi Tanzania jana na kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Carlinhos alitarajiwa kuanza program maalum ya mazoezi leo. Kulingana na kocha Cedric Kaze, hataweza kuwa kwenye msafara wa Yanga jijini Mwanza

Yanga inatarajiwa kuelekea mkoani Mwanza tayari kwa mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Carlinhos anaweza kurejea dimbani mkoani Mara wakati Yanga itakapoifuata Biashara United Oktoba 30

Raia huyo wa Angola amekuwa na mchango mkubwa kwenye mechi za mwanzo katika kikosi cha Yanga akifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’