Tangu kutua kwa kocha Cedric Kaze, kiungo mshambuliaji Farid Mussa amekuwa mchezaji muhimu sana katika kikosi cha Yanga akishiriki michezo yote miwili ambayo Kaze amewaongoza mabingwa hao wa kihistoria
Katika hali ya kushangaza, Farid hakuaminiwa kabisa na kocha aliyepita Zlatko Krmpotic, lakini nyota huyo wa zamani wa Azam Fc, anaonyesha juhudi sana anapokuwa uwanjani
Ushindi wa Yanga katika michezo miwili iliyopita, umechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wake uwanjani
Katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulipigwa uwanja wa Uhuru, Farid ndiye aliyetoa pasi ya bao lililofungwa na Mukoko Tomombe
Lakini pia, hata bao la pili lililofungwa na Waziri Junir katika mchezo dhidi ya KMC, ulikuwa mpira wa kona uliotoka mguuni kwake
Wakati Yanga ikimkosa mtaalam wake wa mipira iliyokufa Carlinhos kutokana na majeruhi, Farid ameweza kuchukua jukumu la kutengeneza nafasi ambazo zimeiwezesha Yanga kushinda mechi zake
Pamoja na haya anayoyafanya, Farid amesema bado hajafikia katika kiwango chake kwani alikaa muda mrefu bila ya kucheza mpira wakati yuko Hispania
Amewaahidi Wanayanga wasubiri mambo mazuri zaidi kutoka kwake