Mabadiliko ya kikosi yalifanywa kimkakati zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2020
Mabadiliko ya kikosi yalifanywa kimkakati zaidi

Yanga imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Gwambina Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa, Misungwi Mwanza

Matokeo haya hayakufurahiwa na baadhi ya mashabiki ambao wametoka kuishuhudia timu yao ikishinda michezo saba mfululizo

Aidha uamuzi wa kocha Cedric Kaze kufanya 'rotation' ya kikosi, umetupiwa lawama lakini bila shaka ni uamuzi uliokuwa na mlengo wa kimkakati zaidi

Ikumbukwe Yanga imekabikiwa na mechi nne katika kipindi cha siku 12

Mechi tatu za mwanzo Kaze hakufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake, leo aliona kuna umuhimu wa kuwapumzisha baadhi ya wachezaji baada ya kucheza mfululizo

Lakini pia ikumbukwe Jumamosi Yanga inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Simba. Pengine ni tahadhari aliyochukua kuwaepusha nyota wake na majeraha

Yanga imesajili wachezaji 25, mabadiliko ya kikosi leo yamewapa fursa wachezaji wengine kuonyesha kile walichonacho kumpa sababu ya kuwapa nafasi

Pamoja na kuwa Yanga haijashinda lakini muhimu zaidi Kaze amethubutu kuwaamini wachezaji wake.

Mara nyingi kwenye mahojiano yake, Kaze amesisitiza kuwa anaunda timu ya wachezaji 11 na sio watu 11.

Wakati ufike kila mchezaji Yanga awe na umuhimu wake, na kuwa mchezaji mmoja akikosekana sio tatizo kwa timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
56m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’