Kisinda kuwakumbushia zile tano tano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2020
Kisinda kuwakumbushia zile tano tano

Msimu wa 2018-19 Simba hawawezi kuusahau katika historia yao kutokana na matukio mawili makubwa

Walifanikiwa kupenya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika. Lakini ilikuwa kama bahati kwani ni msimu ambao walichezea vichapo vizito kwelikweli ugenini

Wakati wakifungwa mabao 5-0 na AS Vita kule DR Congo, winga Tuisila Kisinda alikuwemo uwanjani na alikuwa mfungaji wa moja ya mabao hayo

Lakini pia, Kisinda alimfanya uchochoro mlinzi wa kulia wa Simba Shomari Kapombe

Sasa shoo nyingine ya Kisinda itashuhudiwa kesho pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati huu winga huyo mwenye kasi akiwatumikia Wananchi

Akiwa ndani ya kikosi cha Yanga, msimu huu Kisinda ametoa pasi mbili za mabao na mwenyewe kufunga bao moja

Huyu ndiye mchezaji ambaye walinzi wa Simba wanakuna vichwa ni jinsi gani wataweza kumdhibiti

Safu ya ulinzi ya Simba inaundwa na wachezaji wakongwe hivyo ni wazi kasi ya Kisinda upande mmoja na Farid Mussa upande wa pili itakuwa mtihani mgumu kwao

Kina Feisal Salum na Mukoko Tomombe watakuwa na kazi moja tu, kudondosha mipira nyuma ya mabeki hao ili kina Kisinda wafanye yao...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’