Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema mchezo dhidi ya Simba kesho ni kipimo cha uimara wa kikosi chake msimu huu
Akiwa na takribani wiki tatu tangu alipoanza kuinoa Yanga, Kaze atawaongoza Wananchi katika mchezo huo unotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo mapema leo, Kaze alisema anafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini wamejiandaa kukabiliana nao
"Tunacheza na bingwa mtetezi, unaona utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kukabiliana nao. Mchezo huu utakuwa kipimo cha uimara wa timu yetu msimu huu. Timu iliyokuwepo msimu uliopita ni tofauti sana na hii ya sasa, wachezaji wetu watakuwa na nafasi ya kuonyesha utofauti huo'
"Nafahamu mchezo huu hapa Tanzania una msisimko mkubwa, nawaita mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono wachezaji wao. Tunafahamu ushindi unaweza kutupatia manufaa ya kuongeza tofauti ya pointi kati yetu na Simba," alisema
Hamasa ya mashabiki wa Yanga kuelekea mchezo huo ni kubwa, Wananchi wakiwa na matumani makubwa kwa timu yao kuweza kuibuka na ushindi
Ushindi katika mchezo huo utawaongezea 'gape' la pointi dhidi ya watani zao kufikia alama saba