FT : Yanga 1-1 Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2020
FT : Yanga 1-1 Simba

Mchezo wa kwanza wa watani wa jadi msimu huu ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo Jumamosi, umemalizika kwa Yanga na Simba kugawana pointi baada ya kutoka sare ya bao 1-1

Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 31 likifungwa kwa mkwaju wa penati na Michael Sarpong

Ni baada ya mlinzi wa Simba Joash Onyango kumuangusha Tuisila Kidinda 'TK Master' ndani ya eneo la hatari

Yanga ilitengeneza nafasi kadhaa kwenye kipindi cha kwanza huku ikiwa imara kuwadhibiti Simba eneo la kiungo

Mwanzoni mwa kipindi cha pili nahodha Lamine Moro alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Said Juma Makapu

Katika kipindi cha pili Simba walikuwa bora zaidi na walifanikiwa kusawazisha bao kwenye dakika ya 87 kupitia kwa Onyango ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Mohammed Hussein

Ulikuwa ni mchezo uliotawaliwa na ufundi mwingi, matokeo hayo yanaifanya Yanga iwe mbele ya Simba tofauti ya alama nne

Mabingwa hao wa kihistoria wanaendelea kushikilia nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 24, alama moja nyuma ya Azam Fc inayoongoza ligi ikiwa na alama 25

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
58m ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’