Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kimeondoka mapema leo kuelekea nchini Uturuki kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 dhidi ya Tunisia
Mchezo huo utapigwa Novemba 13 huko Tunisia na timu hizo kurudiana Novemba 17 nchini
Wachezaji saba wa Yanga wamejumuishwa katika kikosi hicho kilichosheheni mastaa kutoka vilabu vya Yanga, Simba na Azam Fc
Metacha Mnata, Deus Kaseke, Bakari Nondo Mwamnyeto, Abdallah Shaibu 'Ninja', Feisal Salum, Farid Mussa na Ditram Nchimbi wamejumuishwa katika timu hiy
ADVERTISE HERE