Novemba 15 mwamba anaanza kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Nov 2020
Novemba 15 mwamba anaanza kazi

Umekuwa mwanzo mzuri sana wa msimu kwa mashabiki wa Yanga ambao wameishuhudia timu yao ikicheza mechi 10 bila ya kupoteza mchezo

Baada ya misimu mitatu ya machozi, jasho na damu, hatimaye msimu huu Wanayanga wanalo la kujivunia kutokana na uimara wa kikosi chao

Habari njema zaidi ni kuwa mambo yataendelea kunoga pale Jangwani kwani kikosi kimeendelea kuimarishwa

Mwezi uliopita Yanga ilitangaza kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza raia wa Burundi ambaye anakuja kuungana na kocha Cedric Kaze ambaye ana asili ya nchi hiyo

Ntibazonkiza anaanza rasmi kuitumikia Yanga Novemba 15 ikiwa ni siku ya kwanza rasmi ambayo mkataba wake unaanza

Nyota huyu atajiunga na mabingwa hao wa kihistoria baada ya kumaliza majukumu na timu yake ya Taifa

Ntibazonkiza ni silaha muhimu sana kwa Yanga, anakwenda kumaliza changamoto katika eneo la ushambuliaji ambalo kasi yake imekuwa ndogo

Ntibazonkiza ni namba 10 asilia, nafasi ambayo ndani ya kikosi cha Yanga imekosa mtu wa kudumu

Inaelezwa GSM pia wamepanga kuongeza mshambuliaji mwingine mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kufunga katika usajili wa dirisha dogo

Injinia Hersi Said anaweza kurejea pale DR Congo kumalizana na ile injini yao ya mabao Jean Mark Makusu

Msimu huu hesabu za Yanga ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu ili kupata tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’