Nahodha msaidizi wa Yanga, kiungo Thabani Kamusoko huenda akarejea dimbani mapema baada ya madaktari kubaini tatizo lake na ameanza matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kamusoko alipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyiwa vipimo awali Yanga ikiwa imejipanga kumpeleka nchini India.
Hata hivyo Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili wamewahakikishia viongozi wa Yanga kuwa mchezaji huyo atatibiwa hapo Muhimbili na majeraha yake yatapona.
Kamusoko amekuwa nje kwa zaidi ya miezi miwili akisumbuliwa na majeraha ya goti.
Yanga inafanya jitihada kuhakikisha wachezaji wake wote wanakuwa timilifu haraka ili kuhakikisha inatimiza malengo yake ya kutwaa ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

ADVERTISE HERE