Omary Chidaba apagawisha mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2020
Omary Chidaba apagawisha mashabiki

Jana Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1

Mabao ya Yanga katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Azam Complex yalifungwa na Tuisila Kisinda, Yacouba Sogne na Michael Sarpong aliyefunga kupitia mkwaju wa penati

Katika mchezo huo kocha Cedric Kaze aliwapa nafasi vijana wanne kutoka timu ya vijana Yanga B

Kivutio zaidi alikuwa kiungo Omary Chibada ambaye aliingia ndani ya dakika 20 za mwisho

Chibada alionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, lakini akiwa mahiri sana katika kupiga pasi

Mashabiki wengi wametamani kumuona kinda huyo anapandishwa moja kwa moja timu ya wakubwa aungane na Adam Kiondo ambaye jana Kaze alimtumia nafasi ya kiungo mkabaji

Kaze hupendelea sana soka la vijana, hivyo bila shaka vijana wengi kutoka Yanga B watanufaika na uwepo wake

Moja ya mambo aliyofanya baada ya kutua Yanga ni kutilia mkazo timu ya vijana, mara kadhaa ametoa maelekezo na mwenyewe kuhudhuria mazoezi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’