Kocha wa makipa wa klabu ya Yanga, Juma Pondamali ameweka wazi swala la mlindalango Deogratius Munish 'Dida' kuwa hatakuwepo Jangwani msimu ujao.
Akihojiwa kwenye kipindi cha michezo cha moja ya redio maarufu jijini Dar es salaam, Pondamali amesema Dida ameachwa na Yanga baada ya mchezaji huyo kutaka kwenda nje kujaribu bahati yake.
Pondamali amesema Dida amegoma kuongeza mkataba hadi atakaporudi kufanya majaribio nje ya nchi. Hivyo Yanga imeamua kuachana nae.
Pondamali amefunguka kuwa Yanga imekamilisha usajili wa Youthe Rostand aliyekuwa kipa wa African Lyon ambaye atasaidiana na Beno Kakolanya.
Yanga pia itaongeza kipa mwingine kutoka kikosi B.

ADVERTISE HERE