Mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili ijayo uwanja wa Benjamin Mkapa, kocha Cedric Kaze huenda akapangua kikosi chake
Kiungo Carlinhos aliyerejea kikosini wiki hii baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua, anaweza kujumuishwa katika kikosi kitakachoshuka dimbani Jumapili
Hii ina maana Yanga wanaweza kuwatumia Mukoko, Fei Toto na Carlonhos pamoja katika mchezo huo
Kabla ya kupata majeraha, Carlinhos alikuwa silaha muhimu kwenye kikosi cha Yanga akifunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao
Kaze amesema kurejea kwake kikosini kumemuongezea machaguo ya wachezaji anaoweza kuwatumia katika mechi za ligi kuu
ADVERTISE HERE