Duma amemaliza kazi Kimataifa, anarejea kuwanyoosha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Nov 2020
Duma amemaliza kazi Kimataifa, anarejea kuwanyoosha

Moja ya sifa kubwa ya mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi 'Duma', ni mchezaji mwenye 'mapafu ya mbwa', ni mpambanaji asiyechoka lakini pia jina la Duma alilipata kutokana na kasi yake awapo uwanjani

Nchimbi ameendelea kuwa mchezaji kipenzi cha makocha wengi licha ya ukosoaji wa hapa na pale kutoka kwa mashabiki

Ni mchezaji ambaye hutumika sana uwanjani, kama hainufaishi timu kwa kufunga moja kwa moja, basi atatoa asisti au hata harakati zake tu zinaweza kupelekea mazingira ya nafasi za mabao kutengenezwa

Juzi alikuwa nguzo muhimu kwenye kikosi cha timu ya Taifa ambacho kililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia

Ndiye mchezaji aliyeisumbua sana ngome ya Tunisia, ilibaki kidogo tu aifungie Stars bao la ushindi kwenye dakika za majeruhi kama sio mpira wake wa kichwa kuikosa tageti kwa sentimita chache tu

Nchimbi pamoja na wachezaji wengine waliokuwa na majukumu ya timu ya Taifa, wamerejea kikosini kujiandaa na mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumapili uwanja wa Benjamin Mkapa

Baada ya kulazimishwa sare katika michezo miwili iliyopita, huu ni mchezo ambao Yanga itahitaji kuondoka na alama zote tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’