Yanga yajipanga kumaliza kibabe duru ya kwanza VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2020
Yanga yajipanga kumaliza kibabe duru ya kwanza VPL

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema mechi saba zilizosalia kumaliza duru ya kwanza ligi kuu ya Vodacom ni muhimu kwa kikosi chake kupata matokeo mazuri yatakayowaweka katika nafasi nzuri katika mbio za kuwania ubingwa

Kaze aliyejiunga na Yanga mwezi uliopita, ameiongoza Yanga katika mechi tano za ligi akishinda mechi tatu na kutoka sare michezo miwili

Ameweka mkakati wa kumaliza duru ya kwanza akiendeleza matokeo bora waliyoanza nayo msimu huu

"Kuna kitu ambacho nafikiria kufanya katika timu,Ukiangalia tuna kama mechi saba hapa za kucheza kumaliza mzunguko wa kwanza ni mechi nyingi ambazo pia zinaweza kubadilisha vitu vingi kwasasa tunataka kuelekeza akili yetu katika mechi hizo," amesema Kaze

Yanga inaanza mchakamchaka wa kusaka alama 21 hapo kesho Jumapili watakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Namungo Fc

Baadae wataelekea kule Chamazi kuikabili Azam Fc, ambao nao wana kikosi bora sana kilichokaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’