Wananchi wana jambo lao kwa Mkapa Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2020
Wananchi wana jambo lao kwa Mkapa Jumapili

Msako wa alama tatu unaendelea kesho Jumapili Novemba 22 pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mabingwa wa kihistoria Yanga watakaposhuka dimbani kuikabili Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 12

Huu utakuwa mchezo wa tatu wa ligi kuzikutanisha Yanga na Namungo Fc, msimu uliopita timu hizo zikitoka sare katika michezo yote miwili

Ule uliopigwa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2, Yanga ikitokea nyuma kwa mabao mawili na kufanikiwa kupata alama moja, shukrani kwa mabao ya David Molinga 'Falcao'

Msimu huu timu hizo zinakutana zikiwa na mazingira tofauti. Yanga itashuka uwanjani ikiwa na morali kubwa tofauti na wapinzani wao, Namungo Fc

Wakiwa kwenye nafasi ya pili, Yanga ndio klabu pekee ambayo bado haijaonja uchungu wa kufungwa msimu huu

Wananchi wenyewe wanasema ndio klabu pekee katika ligi kubwa duniani ambayo haijapoteza mchezo

Baada ya mchezo huo, mchezo utakaofuata kwa Yanga ni dhidi ya Azam Fc. Hivyo ni wazi Wananchi wataingia katika mchezo huo wakiwa na hesabu moja tu, kuondoka na alama zote tatu ili waende Chamazi wakiwa na ari zaidi

Namungo Fc imekuwa na msimu wenye milima na mabonde. Mafanikio waliyopata msimu uliopita, hayaonekani msimu huu

Ni juzi tu wameachana na kocha wao Hitimana Thiery kisha wakamtangaza kocha Hemedi Morocco kumrithi Hitimana

Wanashika nafasi ya tisa wakiwa wamekusanya alama 14 kutoka michezo 10

Hautakuwa mchezo mwepesi lakini ni wazi, kwa Yanga hii ni mechi ambayo wana kila sababu ya kushinda

Wananchi wameaswa kujitokeza kwa wingi kushuhudia tiki-taka la Cedric Kaze ambapo viingilio Mzunguko 5,000/- , V.I.P B & C 10,000/-, V.I.P A 15,000/-, Royal 50,000/-

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’