Kiungo Papi Kabamba Tshishimbi aliyekuwa majeruhi kwa takribani wiki tatu ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga.
Tshishimbi alishindwa kucheza michezo miwili iliyopita dhidi ya Mbeya City na Prisons akisumbuliwa na majeraha ya goti.
Tayari ameungana na kikosi cha Yanga kilichoanza kufanya mazoezi ya Gym jana Jumatatu.
Ligi kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea Disemba 29 ambapo Yanga itasafiri mkoani Mwanza kuivaa Mbao FC.
Yanga bado haijawahi kupata ushindi kwenye uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mbao FC msimu uliopita ilichapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi na pia kombe la FA.
Bila shaka kocha Lwandamina atahakikisha anawaandaa vijana wake kikamilifu ili waweze kuondoka na alama zote tatu Disemba 29.

ADVERTISE HERE