La Liga tayari wamemaliza kazi ya kuandaa mapendekezo ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Yanga
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ameondoka nchini jana kuelekea Hispania ambako atakabidhiwa rasimu hiyo
Mapendekezo hayo yatatoa taswira ya mwelekeo mpya wa mfumo wa uendeshaji klabu ya Yanga
Wanayanga wametakiwa kukaa tayari kupokea mapendekezo hayo na kuunga mkono maamuzi yatakayofikiwa ili kuhakikisha mchakato wa Mabadiliko unakamilika katika wakati uliopangwa
ADVERTISE HERE